Mbeya Institute Of Journalism (MIJO) inakukaribisha katika mwaka wa masomo wa Februari hadi Desemba 2010



Serikali ya Wanafunzi ya Chuo (SOMIJO) inakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika tasnia hii ya Uandishi wa Habari zilizojawa na ukweli zenye kuleta maendeleo kwa mwananchi husika na taifa kwa ujumla.

Tuesday, April 13, 2010

MHINDI WA KAPUNGA ASEMA AWEZA KUUA YEYOTE AKIMKOROFISHA

Na Johnson Jabir/Mike mbughi
MBEYA, TANZANIA

WANANCHI wanaolizunguka shamba la Kapunga Wilayani Mbarali, mkoani Mbeya wamemlalamikia msimamizi wa Shirika hilo Badri Dart kwa unyanyasaji na kusababisha uhasama baina ya wananchi na shirika hilo.

Uchunguzi uliofanywa na JAIZMELA umebaini kuwa kiongozi huyo mwenye asili ya ki-Asia amekuwa mwiba kwa wafanyakazi wa kipato cha chini kwa unyanyasaji na kuwatuhumu kuwa wafanyakazi hao ni wezi.

Baadhi ya wananchi waliofanya mahojiano na JAIZMELA kwa sharti la kutotaja majina yao walisema kuwa tokea Badri ajiunge na kampuni hiyo mwaka 2007 akijitambulisha kuwa yeye ni Afisa mipaka wa shirika hilo amekuwa akizua mitafaruku mbali mbali ikiwemo ya wakazi wa Mapogoro hasa jamii ya wasukuma ambao walidai walipokonywa mashamba yao na mhindi huyo.

Wananchi hao walidai kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwatishia kuua mtu kama wataendelea kupita kwenye mashamba ya shirika hilo wakati ndiyo njia pekee ya kupita kwenda kwenye mashamba yao.

Waliongeza kuwa Badri amekuwa akiwatuhumu na kuwakashfu wananchi hao kuwa ni wezi na kudai kuwa yeye hawezi kutishiwa na mtu yeyote kwa kuwa yuko pamoja na viongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Maheshi Patel.

“Huyu kijana amekuwa akitukashfu sana kwa kusema sisi wakazi wa Kapunga ni wezi, inasikitisha sana maana tupo hapa kapunga mda mlefu hatujawahi kuambiwa na mtu yeyote maneno kama hayo” alisema mzee mmoja jina linahifadhiwa.

“Kwanza amelifanya shirika lichukiwe na wanchi wa eneo hili kwa sababu ya kashifa zake na kauli ya kusema yuko pamoja na viongozi wetu kitu labda kwa kuwa baadhi ya viongozi wanalima kwenye mashamba hayo na akajenga urafiki na viongozi hao ndiyo maana anakiburi” aliongeza mzee mwingine jina linahifadhiwa.

Kapunga bila Badri Dart inawezekana tena kutakuwa na amani nje na hata ndani ya shirika maana hata wafanyakazi wanaendeshwa kama watumwa kwa kweli haiwezekani mtu mmoja akaivuruga kampuni kwa mitafaruku na wananchi, kwanini viongozi wengine wasishutumiwe? Alisema kijana wa Kimasai.

JAIZMELA ilifanya mahojiano na wafanyakazi wa shirika hilo kwa sharti la kutotaja majina yao na kueleza kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwanyanyasa vilivyo na kuwashutumu mara kwa mara kuwa ni wezi huku wengine wakifikishwa mahakamani.

Wafanyakazi hao walisema kuwa amekuwa akiwafanyisha kazi kama watumwa akidai asiyetaka aache kazi zake milango iko iko wazi na kudai kutokana na shida za vibarua ndiyo maana wamekuwa wakivumilia unyanyasaji huo.

“Amekuwa akitutukana matusi na kuwafikisha polisi baadhi ya wafanya kazi akidai ni wezi bila kosa lolote na kwamba anajidai kuwa yeye yu pamoja na viongozi wakubwa hivyo hakuna watakachokifanya juu yake” alisema mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo.

“Tunaomba mtufikishie malalamiko yetu kwa viongozi wa juu ili watambue kwamba sisi watanzania bado ni watumwa licha ya kuwa kuwa tuko kwenye nchi yetu na mtu mmoja tu Badri Dart” alisema mfanyakazi mwingine.

“Ikiwa huyu kiongozi ataondoka ni ukweli kwamba hili shirika litatengamaa ndani na nje ya shirika hili maana hata wananchi wanamlalamikia yeye tu.aliongeza mfanya kazi mwingine.

Hata hivyo kiongozi huyo ambaye aliwahi kufanya kazi katika Hoteli ya kitalii ya Sea Cliff iliyopo jijini Dar es salaam alikana shutuma hizo kwa kudai kuwa ni za uongo.

Baada ya JAIZMELA kuongea na Badri Darti alisema kuwa yeye amekuwa akifuata sheria za shirika na kwamba yeye ni mfuatiliaji makini wa mambo ya kampuni na kudai kuwa hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchukiwa na wafanyakazi na hata wananchi wa nje.

Hata hivyo Badri alikiri kuwafikisha baadhi ya wafanya kazi katika vyombo vya sheria kwa madai ya wizi ingawa alisema kuna wengine kesi zao walishinda na wengine shirika lilishinda huku akisema wengine zinaishia juju tu.

“Asili ya watu wa kapunga ni wezi ingawa wengine wanatushinda kesi na wengine tumeshinda kesi mahakamani ila wengine kesi zao zinaishia juju tu” alisema Badri.

Akizungumzia kutumia uhusiano wake na viongozi wakubwa kuwanyanyasa wananchi pamoja na wafanyakazi wake alisema hiyo si kweli isipokuwa viongozi wameomba mashamba katika shirika lao na kudai wapo pale kama watu wakawaida na si kama mtumishi wa serikali hiyo hizo shutuma ni za uzushi.

Hata hivyo alikiri kuwepo viongozi wakubwa katika mashamba hayo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Jaji Mkuu wa Mkoa Maafisa wa TRA pamoja na Askari 6 ambao wamepewa mashamba katika shirika hilo.

Awali alikana kuwepo na uhusiano wa karibu na kiongozi aliyetajwa kwa jina la Maheshi Patel lakini baada ya kubanwa na maswali alikiri kuwepo na uhusiano na mtu huyo na kudai kuwa ni rafiki yake na baadaye kuwa ni Bwana shamba.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na JAIZMELA umebaini kuwa Maheshi Patel ndiye mwekezaji wa shamba la Kapunga na humtumia Badri dart kama “Technician” pia kama mkaguzi wa ndani wa shirika na utawala.
Posted by JAIZMELA at 14:41 0 comments

Saturday, April 10, 2010

HABARI ZA PASAKA

Na Godfrey Msomba
MIJO


SIKU zote mwanadamu huhitaji kupumzika ili siku inayofuata aweze kufanya vizuri zaidi ya jana hivyo naamini hata wewe umepumzika vya kutosha ili ufanye leo vizuri

KWA LEO INATOSHA.