Mbeya Institute Of Journalism (MIJO) inakukaribisha katika mwaka wa masomo wa Februari hadi Desemba 2010



Serikali ya Wanafunzi ya Chuo (SOMIJO) inakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika tasnia hii ya Uandishi wa Habari zilizojawa na ukweli zenye kuleta maendeleo kwa mwananchi husika na taifa kwa ujumla.

Saturday, May 29, 2010

MZEE PWAGU KATUTOKA


Na Johnson Jabir
MIJO, TANZANIA

Aliyekuwa mwigizaji mahiri redioni Rajab Kibwana Hatia al maaruf Mzee Pwagu amefariki dunia.Mzee Pwagu amefariki Ijumaa, Mei 28, 2010 katika hospitali ya Amana jijini Dar Es Salaam kutokana na kusumbuliwa na kwikwi na hali ya uzee.

Mzee Pwagu alikuwa anakamilisha pacha wake Mzee Pwaguzi katika kipindi cha redio kilichokuwa maafuru sana miaka ya sitini hadi themanini kilichojulikana kwa jina la Pwagu na Pwaguzi.

Kipindi hicho kilikuwa kikirushwa hewani kila siku ya Jumamosi saa kumi na moja na dakika arobaini na tano jioni hadi saa kumi na mbili kamili (11:45 - 12:00) kupitia Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD). Kwa mara ya kwanza kipindi hicho kilianza kusikika mwaka 1966 na kilipendwa kusikilizwa na watu wa rika zote kutokana na kuelimisha na kutoa burudani inayogusa maisha ya kila siku ya Mtanzania, hadi mwaka 1980 kilipokoma.

Marehemu alikuwa akiishi Kigogo Mbuyuni jijini Dar Es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho.Apumzike pema Rajab Kibwana Hatia/Mzee Pwagu.

No comments:

Post a Comment