Na Johnson Jabir
MIJO, MBEYA
Siku kama ya leo miaka 156 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 15 Machi 1854 Miladia, alizaliwa Emil Adolf von Behring tabibu mashuhuri wa Ujerumani. Baada ya kumaliza masomo yake, Behring aliendeleza utafiti wa Louis Pasteur mwanakemia wa Kifaransa katika uwanja wa kuvumbua na kuzuia kuibuka maradhi ya kuambukiza. Kutokana na juhudi zake hizo, mnamo mwaka 1901 kwa mara ya kwanza kabisa alitunukiwa tuzo ya Nobel kwa upande wa tiba. Emil Adolf von Behring alifariki dunia mwaka 1917.
Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita inayosadifiana na 24 Esfand 1358 Hijria Shamsia, ulifanyika uchaguzi wa kwanza wa bunge hapa nchini baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu. Uchaguzi huo ulikata kiu kabisa cha wananchi wa Iran kwa miaka kadhaa ambao waliweza kupiga kura zao kwa uhuru na kuwachagua wabunge wawatakao. Uchaguzi huo ulifanyika huku kukiwa na njama kadhaa za maadui wa Kiislamu ambao walikuwa hawataki kuona demokrasia hiyo ikithibiti hapa nchini.
Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, inayosadifiana na 24 Esfand 1363 vibaraka wanaofungamana na madola ya kibeberu ya magharibi, walitega na kulipua bomu kwenye mkusanyiko mkubwa wa waumini wa sala ya Ijumaa mjini Tehran na kupelekea watu kadhaa kuuawa shahidi na wengine kujeruhiwa. Jambo la kuzingatiwa hapa ni kuwa, mlipuko huo wa sala ya Ijumaa haukusababisha hata kidogo kusimamishwa ibada hiyo, kwani Ayatullah Khamenei aliyekuwa khatibu na Imamu wa sala ya Ijumaa kwa siku hiyo aliendeleza shughuli za ibada hiyo kwa utulivu mkubwa.
Siku kama ya leo miaka 21 iliyopita, inayosadifiana na 15 Machi 1989, ardhi za Taba zilizoko kaskazini mashariki mwa Misri, zilikombolewa baada ya kukaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa miaka kadhaa. Utawala wa Kizayuni wa Israel ulilikalia kwa mabavu eneo la Taba lililoko upande wa mashariki mwa jangwa la Sinai, wakati wa vita vya mwaka 1967. Hatimaye jangwa la Sinai lilirejeshwa kwenye ardhi ya Misri baada ya kutiwa saini makubaliano ya Camp David kati ya Misri na Israel mwaka 1987
No comments:
Post a Comment