Agatha MboyaZAIDI ya Sh 50 billioni zitatumika katika kukamilisha mradi mkubwawa maji unaojengwa katika Jiji la Mbeya.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Uwasa) katika Jiji laMbeya, Simion Shauri alisema mradi huo ulioanza kujengwa Septemba2008 unatarajia kukamilika mwakani na kwamba utawezesha wakazi wote wajiji hilo kupata maji safi na salama katika kipindi chote cha mwaka.
Shauri alisema fedha za ujenzi wa mradi huo wa maji zimetolewa naShirika la Kijerumani KFW pamoja na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) kwakushirikiana na Benki ya Dunia.Kwa mujibu wa maelezo ya Shauri kukamilika kwa mradi huo wa majikutaongeza kiasi cha maji kutoka wastani wa mita 32,000 kwa siku zasasa hadi kufikia mita za ujazo 49,000 kwa siku.
Aliongeza kusema kuwa chini ya mradi huo mkandarasi kutoka nchini UfaransaSogea Satom anajenga mitambo ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kusukumamaji katika vyanzo vya Nkwanana Mwatezi, na LunjiMkandarasi huyo pia anajenga mitambo ya kisasa ya kutibia maji katikavyanzo vya Meta Sisimba, Sai, Lunji, Mwatezi, Iduda na Nsalagapamoja na kujenga vituo vipya vya kusukuma maji katika eneo la SwayaNelotia, Nsalaga na ImetaAlisema matanki saba makubwa ya kuhifadhia maji yanajengwa katikamaeneo ya Veta, Forest mpya, Iwambi, Imeta, Iganjo, Nsoho, na Iduda.
“Mradi huo pia unaongeza mtandao wa maji kwa kuunganisha na mabombayenye urefu wa kilomita zaidi ya 37 na kujenga viungo kwa wateja wapyana kupanua mabwawa ya kutibu maji taka katika eneo la Kalobe ilikuepusha magonjwa ya milipuko kwa wakazi wanaoishi katika maeneohayo,”alisema.
Alisema fedha hizo pia zitatumika katika kununua vitendea kazi kwaajili ya matengezo ya mtandao wa mabomba na shughuli za umeme namagari matatu ya maji taka pamoja na ujenzi wa vyoo mashuleni naujenzi wa vyumba vya kuishi watumishi na ujenzi karakana za kupimausahihi wa dira za maji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Maji safi na Majitakajijini Mbeya, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 80 na zaidiya jumla ya Sh 27 bilioni zimekwishalipwa na gharama za kutekelezamradi mzima ni zaidi ya Sh 56 milioni. Awamu ya pili ya ujenziitagharimu Sh 13 bilioni.