KUTOKA CHUMBA CHA HABARI
WANAFUNZI 27 wa Chuo Cha Uandishi wa Habri Mbeya(MIJO) wanatarajia kufanya mitihani ya kuhitimu Stashahada ya Juu katika Ujuzi wa Habari Jumatatu ya Novemba 8.
Akizungumza katika mahojiano maalum Mkurugenzi wa Chuo hicho Jonas
Mwasumbi alisema kozi hiyo imwetolewa kwa miezi 10 tangu mwezi Februari hadi Novemba mwaka huu.
Alisema kuwa mitihani hiyo ni maalumu kwa kukamilisha stashahada ya
juu ya Fani ya Uandishi wa Habari. Kozi hiyo imejikita katika masuala ya uandishi wa habari katika magazeti, redio na televisheni, maadili katika tasnia ya uandishi wa
habari, upigaji picha na mahusiani katika jamii (Public relations).
Aidha Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa waandishi wa habari nchini
kujikita zaidi katika maadili ya fani hiyo ili kuepusha vurugu na
mafarakano katika jamii.
Imeandikwa na Godfrey Msomba
Kuhaririwa na Johnson Jabir.
No comments:
Post a Comment