Mbeya Institute Of Journalism (MIJO) inakukaribisha katika mwaka wa masomo wa Februari hadi Desemba 2010



Serikali ya Wanafunzi ya Chuo (SOMIJO) inakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika tasnia hii ya Uandishi wa Habari zilizojawa na ukweli zenye kuleta maendeleo kwa mwananchi husika na taifa kwa ujumla.

Saturday, November 6, 2010

JIJI LA MBEYA LAKABILIWA NA UKATA WA MAGARI YA TAKA

Na Onesmo Alfred.

LICHA ya mkoa wa mbeya kuwa jiji lakini bado unakabiliwa na uhaba mkubwa wa magari ya kubeabea takataka jijini hapa .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wakazi wa maaeneo ya Mwanjelwa na Soweto wamesema hali hiyo imekuwa ikiwafanya wao kuwapa kikwazo kutokana na hali ya baadhi ya maghuba kujaa taakataka na nyigine kumwangwa nje.

“Mimi hali hii inanikera sana kwasababu husababisha biashara yangu kwenda vibaya kutokana na wateja wangu kukimbia kutokana na ghuba hili kujaa taka na kutoa harufu kali pia kutokana na biashara yangu ya mamalishe nina somesha watoto watatu wakiwemo wa sekondari wawili na wa shule ya msingi mmoja hivyo kukosa wateja kwangu hunisababishia kukosa ada ya watoto wangu, ”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la mbeya Juma Idd alisema halmashauri ilikuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa magari yakubebea takataka.

Idd alisema hivi sasa halmashauri iko kwenye mikakati yakununua magari ilikuweza kukabiliana na hali hiyo ilikuweza kuufanya mkoa wa mbeya kuwa nahadhi ya jiji na kuwa halmashauri ina mpango wa wakuwa na gari kumi na sita haya niya side roder(yakubebae takataka) na skip master

Alisema halmashauri ilikuwa na magari matatu yakubebea takataka (side roder) likiwepo moja kwaajili ya kubebea maghuba (skip master) ilikuweza kukabiliana na hali hiyo ya kero ya takataka hizo.

Ambapo amesema jiji lina uwezo wakuzalisha tani 1260 kwa siku hivyo gari moja lina uwezo wakubebe safari tatu ambazo ni sawa na tani 14 kwa siku halmashauri ina uwezo wakubeba tani 420 kwa siku

Mkurugenzi alizitaja baadhi ya sababu ambazo husababisha uzalishaji huo wataka kuwa ni idadi kubwa ya watu katika jiji la mbeya likemo lilela kushamili kwa biashara katika jiji la mbeya.

Aidha alisema kuwa jiji la mbeya linashika nafasi ya tatu kwabiashara kitaifa hivyonilahisi sana kuzalisha takataka kwakiasi kibwa ukulinganisha na mikoa mingine nchini.

No comments:

Post a Comment