
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua mbunge wa Hai, Freman Mbowe kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani katika bunge la 10 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbali na kuteuliwa kwa mbunge huyo pia chama hicho kimemteua mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto kuwa makamu wa kambi hiyo bungeni.Hata hivyo uteuzi huo umefanya kambi ya upinzani bungeni kumeguka kwa vyama vingine kutokubaliana na uteuzi huo, na kudaiwa kuundwa kambi mbili za upinzani.Awali Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa usemaji kambi ya upinzani na Aliyekuwa mbunge wa Karatu, Wilbrod Slaa alikuwa naibu wake.
Imeandikwa na :Johnson Jabir
No comments:
Post a Comment