Na Wazo Mboya
ASILIMIA 85 ya watu wenye matatizo ya kusikia (viziwi) hawajaandikishwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Uhuru mwishoni mwa wiki hii Katibu wa Chama cha Viziwi mkoa wa Mbeya(CHAVITA) Today Wilson alisema viziwi wengi hawajaandikishwa katika daftari la kupigia kura kwa kuwa Serikali haijatoa kwa kundi hiloya elimu uraia.
Aliongeza kuwa CHAVITA mkoani Mbeya ina wanachama 3000 lakini walioandikishwa katika daftari ya kupigia kura ni 200.
Hata hivyo aliiomba Serikali na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kuliangalia kundi hilo ili haki ya msingi ya kupiga kura itumike ipasavyo kwa kuandaa maelekezo yatakayowasaidia kupiga kura mwaka huu.
Aidha alisema serikali inaweza kutumia hata mashirika mengine ya umma kusaidia kundi hilo.
No comments:
Post a Comment