Mbeya Institute Of Journalism (MIJO) inakukaribisha katika mwaka wa masomo wa Februari hadi Desemba 2010



Serikali ya Wanafunzi ya Chuo (SOMIJO) inakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika tasnia hii ya Uandishi wa Habari zilizojawa na ukweli zenye kuleta maendeleo kwa mwananchi husika na taifa kwa ujumla.

Wednesday, August 11, 2010

MFUNGO WA RAMADHANI WAANZA

Waislamu duniani jana walianza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan huku wengine wakitarajiwa kuanza kufunga leo alhamisi.

Waislamu wanauanza mwezi wa tisa wa kalenda ya kiislamu ambao hujulikana zaidi kama mwezi wa Ramadhan kwa kujizuia kula na kunywa kuanzia alfajiri jua linapochomoza hadi jioni jua linapozama. Kufunga ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu.Kuanza na kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan hutegemea na kuandama kwa mwezi lakini kumekuwa na mgongano juu ya njia za kugundua kuandama kwa mwezi. Baadhi ya nchi hutaka mwezi lazima uonekane kwa macho na hukataa kutambua kuandama kwa mwezi kwa kutumia njia za kisayansi.

Nchini Saudi Arabia, televisheni ya taifa ya Al-Ekhbariyah ilitangaza kuwa baraza linalohusika na kuthibitisha kuandama kwa mwezi limetoa taarifa kuwa jumatano ndio mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.Nchi za Qatar, UAE, Bahrain, Kuwait, Misri, Syria, Lebanon, Yemen nazo zimetangaza kuwa mwezi wa Ramadhan unaanza leo jumatano.Baraza la Waislamu la Jordan lilitangaza kuwa mwezi haujaonekana nchini humo lakini kwakuwa umeonekana nchi za jirani basi na wao wataanza kufunga leo jumatano.Hata hivyo nchi ya Oman imetangaza kuwa wao wataanza kufunga alhamisi kwakuwa hawajauona mwezi nchi humo.

Licha ya mfungo huo ambao umeanza lakini nchini Pakistan wanauanza kwa machungu ya kupotelewa na ndugu na jamaa waliokufa katika mafuriko ambayo yamesababisha hasara kubwa na watu zaidi ya 1,600 walipoteza maisha.

SOMIJO inawatakia waislamu wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment