Mbeya Institute Of Journalism (MIJO) inakukaribisha katika mwaka wa masomo wa Februari hadi Desemba 2010



Serikali ya Wanafunzi ya Chuo (SOMIJO) inakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika tasnia hii ya Uandishi wa Habari zilizojawa na ukweli zenye kuleta maendeleo kwa mwananchi husika na taifa kwa ujumla.

Tuesday, August 10, 2010

MAANDALIZI LIGI YA TAIFA YAANZA MBEYA


CHAMA cha soka wilaya ya Mbeya Mjini (MUFA) kimeanza maandalizi ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya kwa kusajili timu zitazojiandaa na ligi hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Agosti 28 katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.


Akizungumza Mwenyekiti wa MUFA John Gondwe alisema Ligi ya Taifa ngazi ya wilaya inataka timu zijisajili kwanza kuthibitisha kushiriki mashindano hayo kwa kuanza kuchukua fomu ambazo gharama yake ni Shilingi 90,000.


Pia alizitaja timu ambazo tayari zimechukua fomu za usajili ni Eleven Boys SC, Mwanjelwa Stars, Airport Rangers, Uyole SC, Ilemi SC na Winners SC ambazo zimetoa zimethibitisha kushiriki.


“uchukaji wa fomu unaendelea vizuri ukilinganisha na mwaka jana kwani timu nyingi zimeonyesha moyo wa kushiriki kikamilifu, katika kiasi hicho cha fedha shilingi 20,000 ni kwa ajili ya kadi, shilingi 60,000 ni kwa ajili ya ada ya ushiriki na shilingi 10, 000 ya uanachama wa MUFA”.


Gondwe alitoa wito kwa timu ambazo bado zinasuasua kuthibitisha kushiriki zifanye haraka kwani mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 23, mwaka huu.
Ligi ya Taifa ngazi ya wilaya itamalizika Septemba 31, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment