Mbeya Institute Of Journalism (MIJO) inakukaribisha katika mwaka wa masomo wa Februari hadi Desemba 2010



Serikali ya Wanafunzi ya Chuo (SOMIJO) inakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika tasnia hii ya Uandishi wa Habari zilizojawa na ukweli zenye kuleta maendeleo kwa mwananchi husika na taifa kwa ujumla.

Tuesday, August 10, 2010

MTOTO WA MIAKA 4 AKAMATWA AKIWANGA MBEYA

Mtoto aliyefahamika kwa jina la Midian Obadia(4) amekutwa akiwanga jana majira ya saa 5:00 usiku katika kata ya Igawilo Jijini Mbeya ndani ya nyumba ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mama Sanga.


Mtoto huyo amekutwa akiwa amevaa mfuko wa saruji uliotobolewa juu huku kichwa chake kikionekana kimepakwa vitu vyeupe kama unga, alikusanya watu wa mitaa iliyo karibu .


Pia vitu mbalimbali ambavyo ni sindano,matunguli,mavi ya punda, vitu kama mafuta na barua ambazo zinahusu vikao vya kichawi vitakavyofanyika Jumamosi kwa ajili ya kutathmini vifo vya watu waliowauwa kwa njia ya kuwatoa mimba


Imebainika kuwa Mkazi wa Mtaa wa Mwanyanje kata ya Iganjo iliyopo Uyole jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina Bupe Njoka (54) anadaiwa kumpandikiza uchawi mjukuu wake huyo wa kiume.Bibi huyo anayedaiwa kumpandikiza mtoto huyo uchawi amekana kuhusika na vitendo hivyo ambapo alilazimika kuishi na mtoto huyo baada ya wazazi wake kutengana.


Mwenyekiti wa mtaa huo Antony Mwalyambi alimtaka mtoto huyo aende

No comments:

Post a Comment