MKAZI wa Kabwe Jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Mwakyusa (25) amefariki dunia kwa kupigwa na wananchi wenye hasira juzi majira ya saa 12:45 jioni.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema marehemu alikuwa Mfanyabiashara wa nyama ya bucha ambapo mauti yalimfika baada ya kuiba ng'ombe mmoja jike ambaye thamani yake ni shilingi 900,000/= mali ya mtu aliyefahamika kwa jina la Gwamaka Mwakaselela.
Walisema ng'ombe huyo aliibiwa kwa kuvunja zizi ambapo mara baada hapo alimchukua na kwenda naye maeneo ya Iwambi Jijini humo amabko ndiko walikomchinja na nyama yake waliipakia kwenye gari lenye namba za usajili T746 AAM aina ya Corola iliyokuwa ikiendeshwa na na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Haule Kalamu(26).
Marehemu alifariki muda mfupi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Haule Kalamu ambaye ni dereva wa gari lililopakia nyama hiyo amekamatwa na gari lipo mikononi Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.
Kamanda la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wasijichukulie sheria mkononi kwani ni kosa la kisheria.
No comments:
Post a Comment