
MKAZI aliyefahamika kwa jina moja la Ramadhani ambaye umri wake hakupatikana mara moja amekufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa mwishoni mwa juma majira ya saa 6:15 mchana baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka katika eneo la Mlima Nyoka, Mbeya Vijijini barabara ya Mbeya-Iringa.
Walioshuhudia tukio hilo walisema gari lenye namba za usajili T823 AYZ na tera namba T814 AAS aina ya Leyland lilikuwa likiendeshwa na marehemu, liliigonga gari namba T128 ADY na tera namba T736 ALT aina Scania lililokuwa likiendeshwa na Issa Abdul (34) ambalo lilipoteza uelekeo na kuliigonga gari jingine lilikuwa mbele yake lenye namba za usajili T567 ATS na tera T451 ABF aina ya Scania Tanker lililokuwa likiendeshwa na Gustavu Mwalongo (42) na kupinduka.
Baada ya kupinduka marehemu alikufa papo hapo ambapo utingo wa gari lililosababisha ajali hilo aliyefahamika kwa jina la Saba Kasimu(30) alijeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilisababishwa na gari hilo kushindwa kufunga breki katika mlima huo.
No comments:
Post a Comment